Kuhusu

Soma posti hii kwa dakika 1 (makadirio)

Tangu siku ya kuzaliwa hadi ya kufa mwanadamu amezungukwa na fursa zisizohesabika za kujifunza: Iwe ni shuleni, ama kazini, ama barabarani; ni kutoka kwa watu, katika mazingira ama matukio; kote huko kuna vitu vya kujifunza endapo mhusika atakuwa na nia na mtazamo ulio wazi wa kujifunza.

Kwa ufupi tunaweza kusema MAISHA NI KUJIFUNZA, maana pasipo kujifunza yamkini mwanadamu asingeweza kuishi: baada tu ya kuzaliwa mtoto analazimika kuanza kujifunza vitu mbalimbali vipya – kunyonya, kuwasiliana na mama, n.k. – ili aweze kuishi, na anaendelea kujifunza anavyokua kadri mazingira na wakati unavyodai. Bila shaka ndio maana ubongo (kiungo kikuu katika kujifunza) ndio kiungo kinachokua na kukomaa kwa haraka zaidi ya kingine chochote katika ukuaji wa mwili wa mwanadamu.

Hadi sasa umejifunza nini katika maisha ambacho ungependa wengine nao wajifunze? Yamkini ni vingi. Unaweza kuamua kusambaza upendo kwa kuvishirikisha kwa wengine ili nao wajifunze, ama kuamua kuondoka navyo siku yako ya kuondoka hapa duniani itakapofika. Chaguo ni lako. Na ikiwa chaguo lako ni hilo la kwanza, basi hapa ndo mahala pake: SHIRIKISHA ULICHOJIFUNZA!